Thursday

Habari Picha:Lowassa Akiwa Anachukuwa Kadi Ya Chadema Leo


Mfanyakazi wa uwanja wa ndege amefariki

Mfanyakazi wa uwanja wa ndege huko Abudhabi amefariki baada ya kipita mbele ya injini ya Airbus A380. Boeing 747-8 (a full length double deck vessel) na kuvutwa na hewa....
Sent as received


Zaidi Yao Music Tour


LOWASA : "WATANZANIA.WANATAKA MABADILIKO NA WASIPOYAPATA NDANI YA CCM WATAYATAFUTA NJE YA CCM " MWL J.K.NYERERE

Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania Edward Lowasa ambaye pia alikuwa miongoni mwa waliotangaza nia ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi, leo hii amejiunga rasmi na chama cha upinzani cha CHADEMA. Katika mkutano ambamo amechukua kadi ya chama chake kipya Lowasa amesema alionewa ndani ya CCM, na kusema amejiunga na upinzani kutafuta mabadiliko. Sikiliza matangazo yetu ya hivi sasa kupata zaidi


Msanii MRISHO MPOTO Pamoja Na Timu nzima ya PSPF waingia Mkoani RUVUMA katika Wilaya ya NAMTUMBO

Msanii Mrisho mpoto leo ametembelea Baadhi ya shule zilizopo Mkoani Ruvuma katika Wilaya ya Namtumbo kiijiji alipozaliwa

Hii ni kwa msukumo na msaada kutoka PSPF katika jicho lingine la kuitazama Elimu ikiwa kama chanzo na mwanzo mzuri kwa kizazi kijacho

Misaada hiyo iliyotolewa na Mrisho Mpoto akiwa kama balozi wa PSPF ni pamoja na vifaa vya shule na vitendea kazi kwa wanafunzi hao a shule za msingi.


Wednesday

Zoezi la kujiandikisha katika BVR limekuwa na Matukia mbalimbali

Wakati zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa njia ya BVR likiendelea katika maeneo mbalimbali Dar kumekuwepo na matukio mbalimbali..jana mama kupigwa na mume wake baada ya kuchelewa

Tukio la mtoto wa miaka mitatu kupotea wakati mama yake alipokwenda kujiandikisha maeneo ya Bunju.

Aliporudi nyumbani akamkuta mtoto mmoja mwingine hayupo na mara ya mwisho alionekana kwenye kituo cha daladala akiwa na dada mmoja.

Baadaye alipigiwa simu na mtu mmoja kutoka Mbezi ya Kimara na kuambiwa mtoto wake kapatikana kwa dada mmoja ambaye alidanganya jina la mtoto na kusema ni wa rafiki yake.


HAPA KUNA PICHA 5 ZA LOWASSA NA MKEWE WAKIKABIDHIWA RASMI KADI ZA CHADEMA

Mhe. Freeman Mbowe (katikati) kulia kwake ni Regina Lowassa (mke wa Lowassa) na kushoto kwake ni Edward Lowassa baada ya kukabidhiwa kadi cha Chadema.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,  James Mbatia akimpongeza Edward Lowassa punde baada ya kujiunga na CHADEMA chama kimojawapo kinachounda umoja wa UKAWA.

Mke wa Edward Lowassa, Regina Lowassa akikabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba akimpongeza Mhe. Edward Lowassa baada ya kujiunga na CHADEMA chama kimojawapo kinachounda umoja wa UKAWA.


MSANII WA BONGO MOVIE WASTAR AFURAHIA KUPIGWA CHINI UBUNGE


BAADA ya kupigwa chini katika kinyang’anyiro cha kuwania Ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM Morogoro Vijijini, staa wa filamu Bongo, Wastara Juma ametoa kituko cha mwaka baada ya kusema amejisikia vizuri kwa madai kuwa atapata muda wa kujipanga zaidi.Posted via Blogaway


Kaimu spika job ndugai amwaga bakora za kutosha kwa mgombea mwenzie


Jina la mlalamikaji-Joseph Elieza, Mtuhumiwa Job Ndugai.. Kosa shambulio la kudhulu mwili. Ambapo alimushambulia kwa kumpiga kwa fimbo na ngumi sehemu za tumboni na kichwani. Namba ya kesi ni KNG/IR/547/2015.Tukio limetokea huko kata ya ugogoni wakiwa kwenye mkutano wa kampeni ambapo wote wawili ni watia nia kwa tiketi ya CCM Jimbo la kongwa.


Sunday

Ubunge viti maalum, keisha aula


            Khadija Shaban “Keisha”
Wakati Wema Sepetu akiangukia pua katika kinyanganyilo cha kuwania ubunge wa viti maalum msanii mwenzake wa nyimbo za bongo Fleva Khadija Shaban “Keisha” ambaye pia ni mlemavu wa ngozi ameshida kura za maoni za ubunge wa viti maalum kupitia chama cha Mapinduzi huko Dodoma

Saturday

BARRACK OBAMA AWASILI NCHINI KENYA

HABARI,MICHEZO,BURUDANI NA UDAKU
Rais wa Marekani, Barack Obama akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta leo. Pamoja nae ni Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta. Obama aliwasili nandege yake ya Air Force One.
Rais wa Marekani, Barack Obama akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta leo. Pamoja nae ni Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
Mtoto Joan Wamaitha, 8, ndiye Mkenya wa kwanza kumkaribisha Rais Barrack Obama nchini humo kwa kumpa shada la maua na kupiganae picha kadhaa za kumbukumbu kabla ya kwenda kulakiwa na mwenyejiwake Rais Uhuru Kenyatta.
 Rais wa Marekani, Barack Obama akisalimiana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta leo. 
Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na dada yake Auma Obama huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwaangalia.
 **************
Ndege iliyombeba rais obama ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili za usiku.
Alipowasili Rais Obama amelakiwa na mweyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
mwendo wa saa mbili na robo rais Obama alitua ndege yake.
Alipowasili alizungumza kwa muda mfupi na mwenyeji wake Rais Kenyatta na kisha kutia saini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka.
Obama sasa ameandikisha historia ya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani, kuzuru Kenya akiwa ofisini.
Obama anatarajiwa kufungua mkutano wa sita wa kimataifa kuhusu ujasiria mali katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.
Baadaye rais huyo atafanya mashauriano na Rais Uhuru Kenyatta, Ikulu ya Nairobi.
Siku yan Jumapili rais Obama atahutubia mkutano wa wakuu wa mashirika ya kijamii katika chuo kikuu cha Kenyatta kabla ya kuhutubia mkutano mwingine kwa wakenya wote katika uwanja wa Kasakani.
Obama anatarajiwa kuondoka siku ya Jumapili kuelekea nchini Ethiopia. Source:BBC Swahili & AFP

BVR DAR YAENDELEA KUWA PASUA KICHWA!

HABARI,MICHEZO,BURUDANI NA UDAKU
BVR22(1)
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam, unaendelea pamoja na kujitokeza kasoro kadhaa, ikiwa na pamoja na baadhi ya watu kutumia mbinu mbalimbali ili kukwepa foleni.
Katika Kituo cha Bwawani Shule, Mtoni Kijichi, wanawake wawili waliojifanya wajawazito, walibainika kufanya udanganyifu huo huku mmoja akiwa tayari amejiandikisha.

Shuhuda wa tukio hili alishuhudia mzozo huo baada ya wasichana wawili kupitishwa kutokana na hali zao.
Hata hivyo, mmoja wa majirani ambaye anawafahamu, alidokeza kuwa anawafahamu wasichana hao na hawakuwa na wajawazito.
Mmoja alikuwa amekwishajiandikisha na aliwahi kuondoka mapema kabla ya mwenzake aliyekuja kwa staili hiyo na kushtukiwa.
Baada ya mzozo huo, aliondoka taratibu eneo la tukio ndipo baadhi ya watu walipoanza kumkimbiza kubaini iwapo ni mjauzito au la.
Kuona hivyo, msichana huyo, aliyatoa makaratasi aliyokuwa ameyafunga tumboni mithili ya ujauzito na kuyatupa, huku akikimbia na kutokomea katika vichochoro vya Mitaa ya Mtoni Kijichi.
Mmoja wa wasimamizi wa kituo hicho, alisema kuwa hawana kawaida ya kuwakagua isipokuwa wanachoangalia ni hali za watu wakiwamo wajawazito, walemavu, wazee na wenye watoto wachanga.
Mbali na kasoro hiyo, baadhi ya vituo vya kuandikisha wapigakura vimeongezewa mashine za BVR ili kukabiliana na ongezeko la watu katika vituo hivyo kabla ya kazi hiyo kufungwa Julai 31.
Hata hivyo, bado kuna msongamano mkubwa wa watu katika vituo vingi na kusababisha baadhi yao kupigana kwa waliochukua namba na wale ambao ni wapya.
Vituo kadhaa Jimbo la Temeke vimeonekana kuwa na msongamano mkubwa wa wananchi licha ya kuongezewa mashine.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtoni, Kata ya Mtoni, Omary Mateso alisema kadiri siku zinavyokwenda ndivyo kasi ya uandikishaji inavyoongezeka. Alisema siku ya kwanza waliandikisha watu 495 na siku ya pili watu 587.
Mwandishi msaidizi katika Kituo cha Shule ya Msingi Mtoni, Abdallah Luambano alisema kutokana na mwitikio wa wananchi, waliamua kuomba mashine nyingine ili kuongeza ufanisi.
“Changamoto tunayokabiliana nayo ni kuharibika kwa mashine au wakati mwingine kushindwa kusoma alama za vidole vya baadhi ya watu hasa wanawake kutokana na kupaka mafuta mikononi,” alisema.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbuyuni, Selemani Mpoyo alisema tatizo kubwa lililopo kwenye vituo ni utaratibu unaotumika kuandikisha watu. Alisema jana walikuwa wanaandikisha majina, lakini siku inayofuata watu waliowahi kituoni hawakubali kuanza na majina ya jana.
Katika Kituo cha Shule ya Msingi Kibondemaji, Mbagala, uandikishaji ulikwenda vizuri.
Mwenyekiti wa Mtaa za Zakhem Mbagala, Rajab Masunga alisema walianza na mashine tatu za kuandikisha, lakini kutokana na wingiwa watu wameongezewa nyingine tatu.
Katika kituo cha uandikishaji cha Shule ya Msingi Mbagala, pia mashine ziliongezwa na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbagala, Said Makacha.
Kituo cha Shule ya Msingi Makamba, Temeke mashine pia ziliongezwa sanjari na Kituo cha Shule ya Msingi Makamba, lakini kilielezwa kuwa hakikuwa na utaratibu mzuri wa kuandikisha.

Wema Sepetu ashindwa vibaya kwenye kura za maoni singida viti maalumu

HABARI,MICHEZO,BURUDANI NA UDAKU
11371161_963263657059974_1419755464_n
Wema sepetu ni mmoja ya wasanii waliochukua fomu ya kugombea ubunge viti maalum singida, Leo ilikuwa ni siku ya upigaji wa kura za maoni ambapo Wema Sepetu amekuwa wa mwisho katika matokeo.


Katika matokeo hayo Aysharose Mattembe amepata kura 311, Martha Mlata amepata kura 235, Diana Chilolo amepata kura 182 huku Wema akipata kura 90. Big up Wema kwa kujaribu.

CROSSPOST