Sunday

PICHA / ZA MATUKIO YA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA

CHUMA BLOGMajeruhi. Mungu urehemu tz
ARUSHA.
MKUTANO wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine kujeruhiwa.

Bomu hilo lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhur iwa na mamia ya wananchi.


Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.


Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.


Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.


Watu walioshuhudia tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa bomu hilo lililipuka karibu na jukwaa walilokuwa wamekaa viongozi wa Chadema, wakati Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakiwa katika hatua za kumaliza kuhutubia.


Taarifa zilidai kuwa kuna mtu alionekana akirusha kitu kinachodaiwa bomu kwenye eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa akifuatiliwa baada ya kutokea mlipuko huo, polisi nao walikuwa wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya kutoa machozi na kupiga risasi za moto hali iliyozidisha taharuki.


Baada ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako jukwaani.


Hali hiyo ilifanya barabara zote za mji wa Arusha kujaa watu waliokuwa wakikimbia ovyo.


Hali hiyo ya watu kukimbia ovyo kuliwafanya askari polisi wengi kuingia mitaani kudhibiti watu na hivyo nao kulazimika kutumia mabomu ya machozi hali ambayo ilizidisha taharuki.


Baadhi ya watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na wengine katika Hospitali ya Seliani na wafuasi wa Chadema na watu wengine waliokuwa katika eneo hilo.  
CHANZO MWANANCHI.

10 comments:

Anonymous said...

Hatari sana tunakoelekea ni kubaya,serikali ichukue hatua za haraka na za makusudi kabisa kuiepushia nchi machafuko yanayotunyemelea

Anonymous said...

Tumrudie MUNGU.

Samson Machibya said...

Ee Mungu Baba, tuepushe na hili balaa!

Guydon Makulila said...

serikali yetu iwe makini ktk suala zima la ulinzi na usalama wa nchi yetu vinginevyo tuaogopa kuhudhuria mikusanyiko ya aina yeyote ktk nchi yetu.

Anonymous said...

Viongozi wetu waache kudanganya wananchi kuwa Tanzania tunayo AMANI wakati hali halisi kimatendo inadhilisha vinginevyo. Kwa mtazamo wangu kwa muda tumekuwa na ka-UTULIVU tu lakini nako sasa kanaondoka tena kwa kasi. Ni wakati muafaka sasa umefika Rais atangaze hali ya hatari na hatua za makusudi zichukuliwe kuwakamata wahusika bila kujali dini, vyeo, jinsia, hali za kifedha au kivyama kusudi tuepukane na magaidi hawa wanaohusika.
Nawapa pole wafiwa wote.

Anonymous said...

Arusha kuna nn jamani kila siku matatizo watanzani tuwamke jamani chadema ndio chama chetu tunacho kipenda mku wa mkoa atumtaki na mku wa polis arusha mku wa wilay matatizo ayaisha mara polis wanapiga rahia tumechafukwa na roho tunaitaji mabadiliko kwenye mji wa arusha

Anonymous said...

Haiwezekani ukanieleza kuwa serikali ya Tanzania imeshidwa kutafuta suluhu ya mauaji ya kimyama kiasi hiki,Kunamaswali mengi yakujiuliza kwanza kabisa 1.Serikali ikili kuwa inashiliki katika mauaji yanayo tokea hapa nchini,2.Serikali ijihudhuru kuwapisha wenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu kama akina Adolf Hitle na mwenzake Benito Musolini,3.Jeshi la polisi limeshidwa kufanya kazi?. Nahitimisha kwa kusema hivi Tanzania tumejitafutia maana nyingine ya neno AMANI NA UHURU SI MAANA ILE AMBAYO WOLIPINGANIA AKINA MKWAWA,MILAMBO,KINJINGITILE jini ya Mjerumani na Mwingeleza.

Jane Achimpota said...

jamani wa Tanzania tumwogope Mwenyezi Mungu,taifa letu litalaaniwa kwa kumwaga damu kila kukicha.Hebu tujitahidi kuishi kwa uadilifu,kama wewe hupendi kufa ,vipi kumuua mwenzio?

Anonymous said...

JAMANI HAKUNA MTU ANAEHANGAIKA NA KITU AMBACHO HANA MASILAI NACHO AMA HAFAIDIKI, NA HAKUNA MTU ALIETAYARI KUJIDHURU MWENYEWE HATA SIKU MOJA.HII NI DHAHIRI KUWA ALIEPGA BOMU NI MPINZANI MKUBWA WA CHADEMA NA C MWINGINE WA KUTOKA NJE YA NCHI WALA WAPI NI PAPA TUU ANAJITAHIDI KUTAWALA BAHARI KWA NGUVU ZOTE. LAKINI KWA TAARIFA YAKE NI KWAMBA HATAFIKA MBALI MAANA ANAONYESHA KUKIRI KUWA HANA UWEZO TENA

Anonymous said...

acheni usenge angalieni roho za wa2 hizi mtakuja kudaiwa,RIP KWA WOTE WALIOPOTEZA MAISHA

CROSSPOST