» »Unlabelled » PICHA / MAZISHI YA MFANYABIASHARA BOB SAMBEKE AZIKWA NYUMBANI KWAO MOSHI LEO.

CHUMA BLOG

Mwii wa marehemu Bob Sambeke ukiwa kwenye jeneza tayari kwa mazishi
Jeneza la marehemu Bob Sambeke likwa nje tayari kwa ajili ya kuaga mwli
Mtoto wa marehemu Jamal akifungua jeneza la marehemu baba yake Bob
Jamal akiwa ameshafunua jeneza la baba yake
Watoto wa marehemu Sia na Getrude 
Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea Moshi kuzika
Gari liliokuwa limebeba mwili wa marehemu Bob
Baadhi ya waombolezaji na magari eneo la tukio nyumbani kwa marehemu Njiro, Arusha
Umati mkubwa wa watu ulifurika nyumbani kwa marehemu  “Babu Sambeke” eneo la njiro jijini Arusha  kuuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi .

Taratibu za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi  huku wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka Arusha na Moshi wakionekana kutawala msiba huo.

Magari ya kifahari nayo yalitawala na kusababisha msongamano mkubwa kwenye barabara ya Njiro.

Shughuli hizo zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa katika gari maalumu la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwa ajili ya maziko.

Katika zoezi hilo la kuuaga mwili wa marehemu, Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa marehemu  aliongoza misa ya kumuombea marehemu . 

Ndani ya jeneza marehemu alivishwa nguo zake za urubani.

Tofauti na ilivyozoeleka katika misiba mingine hapa nchini, katika msiba huu watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na  vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia wenyewe, vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi kinywaji hicho.

Marehemu ameacha watoto watatu ambao ni Sia, Jamal na Getruda.

News Source: Wavuti

About salim kilama

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

1 comment:

Leave a Reply

TOA MAONI YAKO HAPA

CHUMA EMPIRE. Powered by Blogger.